Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) – ABNA – Yair Lapid, Kiongozi wa Upinzani wa Israel, alitangaza kuunga kwake mkono mpango wa "Israeli Kubwa" unaotetea kumiliki eneo la Kiarabu kutoka Mto Euphrates hadi Nile, na akadai kwamba "mipaka ya Kibiblia ya ardhi ya Israel imebainishwa."
Lapid alisema: "Mkataba wetu wa umiliki wa ardhi ya Israel ni Biblia, na kwa hiyo mipaka ni mipaka ya Kibiblia."
Lapid alitoa matamshi haya Jumanne katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu matamshi ya Mike Huckabee, Balozi wa Marekani nchini Israel, ambaye alikuwa amesema haoni tatizo kwa Israeli kutawala eneo lote la Mashariki ya Kati.
Lapid aliulizwa: "Huckabee, Balozi wa Marekani nchini Israel, amesema anaunga mkono udhibiti wa Israel wa eneo kutoka Nile hadi Euphrates, na hii ina maana ya kudhibiti Lebanon, Jordan na Syria. Je, wewe unaunga mkono hili au unafikiri linapaswa kusimamishwa?"
Kiongozi wa upinzani alijibu: "Nina hoja yenye msingi wa Kibiblia kuhusu mipaka ya awali ya ardhi ya Israel."
Aliendelea: "Ninaunga mkono kila kitu kinachowapa Wayahudi ardhi kubwa na yenye nguvu na kimbilio salama kwa ajili yetu, watoto wetu na wajukuu wetu. Hiki ndicho ninachokiumga mkono."
Nchi bandia ya Israel ilitangazwa mwaka 1948 katika sehemu ya ardhi ya Palestina, ambayo ilikuwa imekaliwa na magenge ya Kizayuni yenye silaha. Walifanya mauaji ya kimbari na kuwafukuza mamia ya maelfu ya raia Wapalestina. Ukaliaji wa ardhi iliyobaki ulikamilika mwaka 1967 na tangu wakati huo utawala wa Kizayuni umekataa kujiondoa katika ardhi zilizokaliwa na umekataa kuruhusu kuanzishwa kwa dola ya Palestina. Hadi leo, utawala wa Israel haujatangaza mipaka yake ya kujitengenezea.
Your Comment